Alhamisi 1 Januari 2026 - 00:40
Itikafu yapaswa kusalia kuwa kitovu cha kuimarisha maarifa ya kizazi cha vijana

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, kwa kusisitiza umuhimu wa kulinda harakati ya Itikafu, ameielezea ibada hii kuwa ni uwezo wa kimkakati kwa ajili ya kuimarisha maarifa ya kidini, kuilinda fikra na malezi ya kizazi cha vijana dhidi ya mashambulizi ya kifikra na kiutamaduni, na akasisitiza juu ya ulazima wa kupanga mipango kwa mfumo thabiti, kuanzisha rasilimali endelevu na kuimarisha uratibu wa taasisi za hawza katika kuendeleza harakati hii ya kiroho.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu nchini Iran, katika kikao chake na wajumbe wa Kamati Kuu ya I‘tikafu kilichofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu, kwa kusisitiza nafasi ya kimkakati ya I‘tikafu katika uongofu wa kiroho wa kizazi cha vijana, aliitaja ibada hii kuwa ni “nuru inayong’aa na chemchemi inayobubujika ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu”, na akasema: Tunatarajia I‘tikafu ya mwaka huu, kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita, iwe chanzo cha uongofu, kuinuka kiroho na kunufaika kwa kina kizazi cha vijana kutokana na neema ya ukaribu na Mwenyezi Mungu, na sisi sote tuhesabiwe miongoni mwa watumishi wa kweli na waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumuabudu.

Akiashiria kuwa kufanya huduma katika njia ya I‘tikafu ni jukumu la Kimungu na la pamoja, aliongeza kusema: Kimsingi, njia hii si njia ya shukrani na pongezi za kawaida; kwa sababu kazi yenu na yetu ni jukumu la pamoja katika ibada. Pamoja na hayo, ninatoa shukrani za dhati kwa mkusanyiko huu wa watu wasomi, wapendwa na wenye thamani, na pia kwa msafara mkubwa na mpana wa watumishi wa I‘tikafu kote nchini, ambao kwa mapenzi, shauku na ari, wanajitahidi kuendesha kwa fahari zaidi ibada hii ya kiroho. Sisi tunashuhudia kwa karibu kwenye maeneo mbalimbali ya nchi jinsi wananchi wanavyosimama kwa mapenzi makubwa na mshikamano katika kuitumikia misikiti, kufanya ibada na kumdhukuru Mwenyezi Mungu.

Kusisitiza umuhimu wa I‘tikafu kubakia ya wananchi

Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu nchini, akirejelea maoni yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati Kuu ya I‘tikafu, alisisitiza: Kama nilivyokuwa nikisema kila mwaka, kuna mambo kadhaa ya msingi katika njia hii. Jambo la kwanza ni ulazima wa kulinda I‘tikafu ibaki kuwa ya wananchi. Harakati hii lazima ibaki ya wananchi kikamilifu; wananchi kwa uwepo wa watu wema, wenye kujali na waumini. Popote itakapohitajika, kwa ajili ya kulinda uwananchi wa harakati hii na kudumisha kanuni zake za kiroho na kimalezi, nikiwa pamoja na wahusika wa kidini na kitamaduni, niko tayari kutoa huduma na naliona hili kuwa ni jukumu langu.

Akasema: Kazi ya I‘tikafu lazima isonge mbele kwa msingi wa ushiriki wa wananchi. Misaada ya muda mfupi ya wananchi au hata misaada kwa ajili ya kuanzisha rasilimali endelevu haina tatizo, lakini msingi wa kazi lazima ubaki kuwa wa wananchi, na mimi ninasisitiza kwa msisitizo mkubwa juu ya jambo hili.

Ayatullah A‘rafi, katika kuendelea na hotuba yake, alitaja jambo la pili kuwa ni umuhimu wa kuwa na mfumo thabiti na mtazamo wa baadaye katika usimamizi wa I‘tikafu, na akasema: Kazi yoyote inayotaka kukua na kupata maendeleo endelevu, inahitaji misingi, nidhamu, hati, dira, utafiti wa mustakabali, uchambuzi na upangaji wa mipango, bila kupoteza utambulisho wake wa uwananchi. Kwa bahati nzuri, ninyi kwa mtazamo huu mmepiga hatua nzuri, na inahitajika mtazamo huu uimarishwe zaidi.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza za Kielimu, alitaja jambo la tatu kuwa ni juhudi za kuanzisha rasilimali za kifedha endelevu kwa ajili ya I‘tikafu, na akasema: Ikiwa mtaweza kwa kubuni mifumo kama waqfu na rasilimali endelevu, kuunda nguzo ya kudumu kwa ajili ya I‘tikafu, hiyo itakuwa kazi yenye baraka kubwa sana. Hata kama katika njia hii kutahitajika msaada kwa ajili ya kuanzisha rasilimali hizo endelevu, mimi niko tayari kutoa msaada. Inahitajika kubuni mfano unaobadilika na unaolingana na mazingira ya I‘tikafu, ili uweze kuunga mkono harakati hii ya kiroho katika muda mrefu.

Akiashiria hali ngumu ya kifikra ya kizazi cha leo, aliongeza kusema: Kijana wa leo yuko katika mazingira ya mashambulizi makubwa ya habari na fikra kutoka sekta tofauti. Sehemu ya hali hii inatokana na wimbi la kimataifa, na sehemu nyingine ni kwa sababu ya kulengwa mahsusi kwa nchi yetu katika vita tata vya kudhoofisha misingi ya kifikra na kiutambuzi ya jamii. Kwa msingi huo, vijana wanaoelekea katika I‘tikafu ni wenye thamani kubwa sana, na wanapaswa kuthaminiwa ipasavyo.

Ayatullah A‘rafi alisisitiza: Vijana hawa wanapaswa kuimarishwa na kuthibitishwa kielimu na kima‘rifa, na pia kulelewa kama wahubiri na wajumbe wa kitamaduni na kiroho; kwa namna ambayo wao wenyewe wawe askari na majeshi ya thamani za Kimungu na I‘tikafu. Jambo hili linahitaji mipango maalumu, kuwatambua wenye vipaji miongoni mwa walioko katika I‘tikafu, na kuweka mazingira ya ushawishi wao katika jamii. Sambamba na hilo, ni lazima pia kuweza kuufikisha ujumbe wa I‘tikafu hatua kwa hatua kwa wale ambao bado hawajaingia katika njia hii; kazi ngumu inayohitajia fikra, sanaa na mipango mahsusi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha